Klabu ya Azam FC imefuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kwa mara ya kwanza tabgu klabu hiyo kuanzishwa miaka 21 iliyopita kufuatia ushindi wa jumla wa 9-0 dhidi ya KMKM Fc kwenye hatua ya pili ya CAFCC.
Azam Fc ilishinda 2-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kabla ya Kusini 7-0 kwenye marudiano katika dimba la Azam Complex, Chamazi na kuandika historia.

