Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imevitaka Vyama vya siasa na wafuasi wake kufanya kampeni za kistaarabu ili kudumisha amani na mshikamano uliopo.
Hayo yameelezwa leo Julai 27,2025 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa Kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Vyama vya siasa kuhusu uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa juu wa vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba,Mwenyekiti wa Chaumma,Hashim Rungwe na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Addo Shaibu.
“

