Dortmund wafuzu ligi ya Mabingwa

Dortmund wafuzu ligi ya Mabingwa

Borussia Dortmund itacheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya ushindi wa 3-0 nyumbani dhidi ya wachezaji Holstein Kiel iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani siku ya Jumamosi.

Wakiwa katika nafasi ya 11 wiki saba tu zilizopita, Dortmund walikusanya pointi 22 kati ya 24 katika mechi zao nane za mwisho za ligi, wakipanda hadi nafasi ya nne, wakiwapita Freiburg waliopoteza 3-1 nyumbani dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Dortmund, ambao hawakuwa kwenye nne bora tangu mwezi Septemba, walianza vyema dhidi ya wapinzani wao ambao tayari wameshuka daraja wakati Serhou Guirassy alipofunga penalti dakika ya tatu.

Wakijua walihitaji ushindi mnono ili kuhakikisha wanamaliza katika nne-bora, matumaini ya Dortmund yalionekana kuwa mazuri wakati Marcel Sabitzer aliongeza bao la pili kwa shuti la chini chini dakika mbili baada ya kipindi cha mapumziko na Felix Nmecha akafunga bao la tatu dakika 73 zikiwa zimepita.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *