Klabu ya Azam imefikia makubaliano ya kuachana kocha Yousouph Dabo pamoja na wasaidizi wake rasmi kuanzia Septemba 03,2024.
Dabo aliyefanya kazi Azam kwa mwaka mmoja, anaondoka na wasaidizi wake.
Hii ni kufuatia kutopendezwa na mwenendo wa klabu hiyo.
Mbali na kutoanza vizuri, Azam pia wametolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

