Bruno Fernandes Ang’ara Chelsea Ikiangukia Pua Nyumbani

Bruno Fernandes Ang’ara Chelsea Ikiangukia Pua Nyumbani

Manchester United imepiga hatua kubwa kuelekea kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) msimu ujao baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea katika dimba la Stamford Bridge. Bao pekee la Matheus Cunha katika kipindi cha kwanza liliwatosha “Mashetani Wekundu” kutanua pengo la alama kumi dhidi ya Chelsea waliopo nafasi ya sita, zikiwa zimesalia mechi tano pekee za Ligi Kuu ya Uingereza kumalizika.

Mchezo huo ulianza kwa presha kubwa kutoka kwa Chelsea, ambapo Enzo Fernandez alikosa nafasi ya wazi akiwa ana kwa ana na kipa Senne Lammens. Chelsea walidhani wamepata bao kupitia kwa Liam Delap, lakini mwamuzi alikataa bao hilo kwa kuotea. Katika dakika ya 43, kinyume na mchezo unavyokwenda, Bruno Fernandes alifanya kazi ya ziada pembeni na kumpasia Cunha aliyepigilia msumari wa ushindi.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *