Biden, Trump wamlilia Jimmy Carter

Biden, Trump wamlilia Jimmy Carter

Rais Joe Biden na Rais mteule Donald Trump wameongoza ibada ya Rais wa zamani wa Marekani na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Jimmy Carter, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 100.

Carter, ambaye aliishi muda mrefu kuliko rais yeyote katika historia nchini humo, alifariki Jumapili alasiri nyumbani kwake huko Plains, Georgia.

Biden alimtaja marehemu kama “mtu wa kanuni, imani na unyenyekevu,” wakati Trump alisema Wamarekani wote wanadaiwa deni la shukrani na kiongozi huyo.

Carter , aliyekuwa mkulima wa karanga , alikuwa rais mnamo 1977, kabla ya kulazimishwa kuondoka Ikulu ya White House baada ya muhula mmoja tu wa miaka minne wakati Ronald Reagan alipoibuka na ushindi katika uchaguzi uliofuata.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *