Amorin kuwabeba wachezaji waliokosa soko

Amorin kuwabeba wachezaji waliokosa soko

Meneja wa Manchester United Ruben Amorim amesema yuko tayari kuwajumuisha tena wachezaji wa klabu hiyo katika kikosi chake iwapo hawataweza kuuzwa kwa ada zinazolingana na hesabu zinazotarajiwa na mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Alejandro Garnacho, Jadon Sancho, Antony na Tyrell Malacia wameondolewa kwenye kikosi kilichosafiri kuelekea Marekani kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya wa klabu hiyo wakitafuta uhamisho kutoka Old Trafford.

Lakini ingawa wamelazimika kufanya kazi tofauti na kikosi cha kwanza tangu United warudi mazoezi kabla ya msimu mpya, Amorim alikiri kuwa atakuwa tayari kuwakubali wachezaji hao kurudi kwenye kikosi chake iwapo hawatauzwa.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *