Wakili auawa kwa kupigwa risasi Msumbiji

Wakili auawa kwa kupigwa risasi Msumbiji

Wakili wa kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini Msumbiji ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu Maputo pamoja na afisa wa chama kimoja.

Elvino Dias alikuwa wakili wa Venâncio Mondlane, ambaye aligombea urais wa Msumbiji akiwakilisha chama cha siasa cha Podemos katika uchaguzi wa siku 10 zilizopita.

Dias alifariki akiwa na afisa mwenzake wa Podemos Paulo Guambe wakati watu wenye silaha waliposhambulia gari lao.

“Waliuawa kikatili [katika] mauaji ya kinyama,” lilisema shirika la haki za mitaa la Kituo cha Demokrasia na Haki za Kibinadamu (CDD).

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *