Stone aipa City ushindi dhidi ya Wolves

Stone aipa City ushindi dhidi ya Wolves

Beki wa Manchester City John Stones amefunga kwa kichwa bao la ushindi wa dakika za mwisho katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers Jumapili na kuwaweka kileleni mwa Ligi ya Premia na kuweka rekodi ya klabu ya mechi 31 za ligi bila kufungwa.

Kwa ushindi huu, City wamesonga kileleni kwa tofauti ya mabao wakiwa na pointi 20, mbili juu ya Liverpool ambao pia wanamenyana na Chelsea.

Wolves wako mkiani kwa pointi moja na hawajapata ushindi wowote msimu huu

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *