5 wauwa kwa mawimbi makali Australia

5 wauwa kwa mawimbi makali Australia

Watu watano wamekufa maji baada ya mawimbi makubwa kupiga sehemu za Australia mwanzoni mwa wikendi ya Pasaka.

Wengine wawili hawapatikani katika ufuko wa New South Wales na majimbo ya Victoria.

Siku ya Jumamosi mwili wa mwanamume mmoja ulipatikana kwenye maji karibu na Tathra kusini mwa New South Wales.

Tukio hili limejiri siku moja baada ya mvuvi mwenye umri wa miaka 58 na wanaume wengine wawili kupatikana wakiwa wamefariki katika matukio tofauti katika jimbo hilo.

Waokoaji wanamtafuta mwanamume aliyesombwa na maji karibu na mji mkuu wa Sydney.

Pia siku ya Ijumaa, mwanamke mmoja alikufa maji na mwanamume mmoja hajapatikana baada ya kundi lao kusombwa na bahari huko San Remo huko Victoria.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *