Zaidi ya Wapalestina 50,000 wameuawa wakati wa kampeni ya kijeshi ya Israel huko Gaza, Wizara ya Afya ya eneo hilo inayosimamiwa na Hamas imetangaza.
Idadi hiyo – 50,021 – ni sawa na karibu 2.1% ya wakazi milioni 2.3 kabla ya vita katika eneo hilo.
Jumla ya watu wengine 113,274 wamejeruhiwa katika kipindi kama hicho, wizara hiyo ilisema.
Takwimu kutoka kwa Wizara ya Afya ya Gaza (MoH) zimetumika sana wakati wote wa vita na zinaonekana kuwa za kuaminiwa na Umoja wa Mataifa (UN) na taasisi za kimataifa.
Lakini Israel imekanusha mara kwa mara data zilizochapishwa na mamlaka ya Gaza.

