Wanafunzi 29 wafariki kwa mshtuko

Wanafunzi 29 wafariki kwa mshtuko

Watoto 29 waliokuwa wakifanya mitihani yao ya shule katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameuawa kwa mshituko baada ya mlipuko uliotokea karibu na hapo kusababisha hofu, mkurugenzi wa hospitali aliambia BBC.

Mlipuko huo, katika siku ya pili ya fainali za shule za upili siku ya Jumatano, ulitokea kwenye transfoma ya umeme, alisema Abel Assaye kutoka hospitali ya jamii ya Bangui.

“Kelele za mlipuko, pamoja na moshi” zilisababisha taharuki miongoni mwa takriban wanafunzi 6,000 waliokuwa wamekaa katika shule moja katika mji mkuu, Bangui, kituo cha redio cha eneo hilo Ndeke Luka kiliripoti.

Rais Faustin-Archange Touadéra ametangaza kipindi cha maombolezo ya kitaifa kufuatia tukio hilo.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *