Uganda imetuma vikosi maalum katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kumsaidia Rais Salva Kiir kuulinda mji huo.
Mkuu wa jeshi la Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema juu ya mpango huo.
Hatua hiyo imekuja huku mvutano ukiongezeka kati ya Kiir na naibu wake Riek Machar, jambo linalozua hofu kwamba makubaliano yao tete ya amani yanaweza kusambaratika na mzozo unaweza kuanza tena.
Jenerali Kainerugaba hakutoa sababu za kutumwa wanajeshi wa nchi hiyo katika jimbo hilo jirani, lakini alisema kuwa hatua yoyote dhidi ya Kiir “ni tangazo la vita dhidi ya Uganda”.
“Tutalinda eneo lote la Sudan Kusini kama kama eneo letu vile,” aliongeza kwenye mtandao wa kijamii.

