Uchaguzi Mkuu nchini Uganda unategemewa kufanyika kati kati ya mwezi Januari, 2026.
Hii ni kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda.
Rais wa sasa aliyeko madarakani kwa zaidi ya miongo 4 Yoweri Museveni anagombania tena kuongeza muda wa utawala wake hadi kufikia karibu nusu karne katika uchaguzi huo.
Hata hivyo, anategemewa kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

