Trump alionya kundi la Hamas

Trump alionya kundi la Hamas

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa kile alichokiita “onyo la mwisho” kwa Hamas kuwaachilia mateka raia wa Israel inaowashikilia huko Gaza.

“Nitaitumia Israel kila inachohitaji ili kumaliza kazi, hakuna hata mwanachama mmoja wa Hamas atakayesalimika ikiwa hamtafanya kama ninavyosema,” Trump alisema katika chapisho refu kwenye mitandao ya kijamii.

Hamas ilimshutumu rais huyo wa Marekani kwa kuihimiza Israel kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano yanayotekelezwa hivi sasa kati ya pande hizo mbili.

Pia imelaani kauli hiyo ya Trump na kusema kuwa inarudisha nyuma mpango wa kusitisha vita.

Kauli ya Trump imekuja saa chache baada ya Ikulu ya White House kuthibitisha kuwa inafanya mazungumzo ya moja kwa moja na Hamas kuhusu mateka waliosalia.

Washington hadi sasa imeepuka kujihusisha moja kwa moja na kundi hilo, na kuna sera ya muda mrefu ya Marekani inayoizuia kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na taasisi inazoziorodhesha kama mashirika ya kigaidi.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *