Israel imekubali “masharti ya lazima” ili kukamilisha usitishaji vita wa siku 60 huko Gaza, Rais wa Marekani Donald Trump amesema.
Kupitia andiko lake kwenye mtandao wa Kijamii, Trump alisema kuwa wakati wa usitishaji mapigano uliopendekezwa umefika na pande zote zimekubaliana kumaliza Vita”.
” Natumai kwamba Hamas itayapokea makubaliano haya,” amesema.
Hata hivyo, Israel haijathibitisha kukubaliana na masharti ya makubaliano.
Afisa wa Hamas aliambia BBC kuwa kundi hilo “liko tayari na makini” kufikia makubaliano ya kumaliza vita hivyo.

