Taifa Stars yajipanga kuanza vyema AFCON dhidi ya Nigeria

Taifa Stars yajipanga kuanza vyema AFCON dhidi ya Nigeria

Taifa Stars ipo katika hali ya kujiamini na morali ya juu kuelekea mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Nigeria, utakaochezwa kesho Desemba 23, 2025, mjini Fez, Morocco.

Taarifa kutoka kambini zinaeleza kuwa kikosi cha Taifa Stars kimekuwa kikifanya mazoezi makali jijini Sale, Rabat, kikilenga kuimarisha mbinu za kiufundi pamoja na kuongeza kiwango cha utimamu wa mwili kwa wachezaji kabla ya mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Imeelezwa kuwa timu itasafiri kwenda Fez, takribani kilomita 202 kutoka Rabat, kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho. Hatua hiyo inalenga kuwapa wachezaji fursa ya kuzoea mazingira ya uwanja utakaoandaa mechi hiyo muhimu ya ufunguzi.

Mashabiki kote nchini wanasubiri kwa hamasa kubwa kuona Taifa Stars wakianza kampeni ya AFCON 2025 kwa ushindi, wakitumaini matokeo chanya dhidi ya wapinzani wao wakali, Nigeria. ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *