Simba Yaendelea Kusuasua CAFCL Baada ya Kupigwa 2-1 na Stade Malien

Simba Yaendelea Kusuasua CAFCL Baada ya Kupigwa 2-1 na Stade Malien

Simba SC imeangukia kipigo cha pili mfululizo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa 2-1 na Stade Malien nchini Mali. Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Machi 26 umeiacha Simba ikiburuza mkia wa Kundi D bila pointi baada ya mechi mbili.

Stade Malien walipata mabao kupitia Nkeng dakika ya 16 na Simpara dakika ya 23, kabla ya Clatous Chota Chama ‘Maema’ kupunguza bao dakika ya 54. Licha ya jaribio hilo, Mnyama alishindwa kusawazisha hadi mchezo ukaisha.

Katika msimamo wa kundi, Petro Atletico wanaongoza kwa pointi 4, wakifuatiwa na Stade Malien wenye 4, na Esperance ikiwa nafasi ya tatu kwa alama 2, huku Simba ikifungia orodha na 0.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *