Klabu ya Simba imewasili Zanzibar kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya siku chache zilizobaki kuelekea Mechi ya hatua ya nusu fainali ya Mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika #CAFCC dhidi ya Stellenbosc ya Afrika kusini, Aprili 20, 2025 katika Dimba la New Amaan Complex, Unguja, Zanzibar.
Simba imefuzu hatua hiyo baada ya kuwaondoa Al Masry ya Misri jijini Dar es Salaam.

