Serikali, wadau kupanda miti Bilioni 1 kunusuru theluji Mlima Kilimanjaro

Serikali, wadau kupanda miti Bilioni 1 kunusuru theluji Mlima Kilimanjaro

Serikali kwa kushirikiana na wadau ina mpango wa kupanda miti bilioni moja katika mikoa ya Kaskazini, ukiwemo mkoa wa Kilimanjaro ili kusaidia uhifadhi wa theluji katika mlima Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amesema lengo ni kunusuru theluji inayotoweka katika Mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.

Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeanzisha kampeni maalumu ya kupanda miti zaidi ya Bilioni katika kanda hiyo inayojumuisha mikoa ya Tanga, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Kati ya idadi hiyo, miti takribani Milioni nane itapandwa katika Mkoa wa Kilimanjaro ili kunusuru theluji hiyo.
 
Naibu Waziri Kitandula ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi aliyetaka kujua hatua mbalimbali za kuinusuru theluji hiyo na uhifadhi wa mazingira.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *