Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys imefungwa 4-1 na Zambia katika michuano ya AFCON U-17 inayoendelea nchini Morocco.
Hadi mapumziko, Zambia walikuwa wanaongoza 2-0.
Kipindi cha pilli, waliruhusu mabao mengine kabla ya kupata la kufutia machozi.
Matokeo haya ni mwanzo mbaya kwa kikosi cha kocha Agrey Morris, ambao sasa watalazimika kujipanga kwa mchezo wao wa pili dhidi ya Uganda, ambayo nayo ilipoteza kwa mabao 5-0 dhidi ya wenyeji Morocco.

