Salah: Trent Arnold hastahili kuzomewa

Salah: Trent Arnold hastahili kuzomewa

Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah alisema Trent Alexander-Arnold, ambaye anatazamiwa kuondoka baada ya miaka 20 toka ajiunge na klabu hiyohastahili kuzomewa na mashabiki hata kidogo

Salah, ambaye anaongoza ligi akiwa na mabao 28 akiwa na mabingwa Liverpool msimu huu, alisema Alexander-Arnold anastahili kuagwa ipasavyo baada ya yote aliyoifanyia klabu yake ya utotoni.

“Nadhani kwa namna fulani mashabiki walikuwa wakimchukia.,”

” Lakimi mashabiki walimstahili kumtendea haki,” Salah aliambia Sky Sports katika mahojiano yaliyochapishwa Ijumaa.

“Nilishangaa kwa sababu hivi sivyo tunavyofanya kama mashabiki wa Liverpool…fikiria mtu ambaye anakupa kila kitu kwa miaka 20. Haipaswi kuwa hivi. Natumai hilo litabadilika katika mchezo ujao, dhidi ya Brighton au katika mchezo wa mwisho wa msimu, kwa sababu anastahili kwaheri ya heshima,” amesema Salah

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *