Ruben Amorim amesema ana imani na Mason Mount

Ruben Amorim amesema ana imani na Mason Mount

na kwamba kiungo huyo wa zamani wa Chelsea anatamani sana kufanikiwa katika klabu ya Manchester United baada ya kusumbuliwa na majeraha Old Trafford .Mount, 25, alijiunga na United Julai 2023 kwa mkataba wa awali wa pauni milioni 55 lakini ameichezea klabu hiyo mara 28 tu, akifunga bao pekee.

Siku ya Alhamisi mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alianza mechi yake ya kwanza tangu Agosti, akicheza takriban saa moja katika ushindi wa 3-2 wa United dhidi ya Bodo/Glimt kwenye Ligi ya Europa.

“Jambo la kwanza ni kwamba anafanya kazi kwa bidii sana,” Amorim alisema,”

“Nina imani atafanya vizuri sana na kuisadia timu,” amesema.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *