RAIS TINUBU AMFUKUZA WAZIRI WA FEDHA

RAIS TINUBU AMFUKUZA WAZIRI WA FEDHA

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, amemfuta kazi Waziri wake wa Fedha na kumteua mtaalamu wa masuala ya kodi kuchukua nafasi hiyo, katika hatua inayolenga kuimarisha uungwaji mkono wa mageuzi yake makubwa ya kiuchumi.

Wale Edun, mwenye umri wa miaka 70, ambaye aliwahi kuwa kamishna wa Fedha wakati Tinubu alipokuwa Gavana wa Jimbo la Lagos kati ya mwaka 1999 na 2004, ameondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Taiwo Oyedele, mwenye umri wa miaka 50, aliyewahi kufanya kazi katika kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC) kama mtaalamu wa kodi.

Oyedele alikuwa amerejea Serikalini kama Naibu Waziri wa Fedha Machi 16, na alichukua jukumu muhimu katika mageuzi ya mfumo wa kodi ya Serikali ambayo yalianza kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa Edun anatakiwa kukabidhi majukumu yake kabla ya Aprili 23, huku mchakato wa makabidhiano ukitarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa siku ya kazi siku ya Alhamisi.

Waziri huyo alikuwa akionya kuhusu athari za viwango vya juu vya riba katika nchi zinazoendelea, akisema vinaweza kudhoofisha mafanikio ya mageuzi ya kiuchumi.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *