Rais Samia Suluhu Hassan amesema itakuwa vyema uwanja wa Suluhu visiwani Zanzibar kutumika katika michuano ya Afrika ya Ligi za ndani (CHAN) inayotarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar mapema mwaka 2025.
Akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja huo uliopo Kizimkazi, Kusini Unguja Rais Samia amesema kukamilika kwa uwanja huo kutaifanya iweze kuwa sehemu ya michuano hiyo kwa kufanyika viwanjani hapo.
Lakini pia amesema michuano hiyo itafanyika kwa ufanisi zaidi kwa uwepo wa miundombinu bora zaidi.
Hivyo, amewaagiza viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) na Shirikisho la Soka Zanzibar
(ZFF) kuhakikisha wanakagua maendeleo ya ujenzi huo na kuzingatia vigezo muhimu ili kukidhi sifa

