Polisi wadaiwa kumuua mwanahabari Kenya

Polisi wadaiwa kumuua mwanahabari Kenya

Mwanablogu Mkenya aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi alipigwa kichwani na huenda kifo chake kilisababishwa na kushambuliwa, uchunguzi wa maiti umefichua.

Hii inakinzana na madai ya polisi kwamba Albert Ojwang “alipata majeraha kichwani baada ya kugonga kichwa chake kwenye ukuta wa seli”

Kifo chake kimezua hasira kubwa nchini Kenya, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakitaka polisi wawajibishwe.

Bw Ojwang alizuiliwa kufuatia malalamishi ya naibu mkuu wa polisi, akidai kuwa alimkashifu kwa kumharibia jina kwenye mitandao ya kijamii.

“Sababu ya kifo iko wazi sana; jeraha la kichwa, kubanwa kwa shingo na majeraha mengine yameenea mwili mzima ambayo yanaonesha kushambuliwa,” daktari wa magonjwa ya serikali Bernard Midia alisema.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *