Namibia yapiga marufuku mazishi ya Serikali sababu ya gharama

Namibia yapiga marufuku mazishi ya Serikali sababu ya gharama

Serikali ya Namibia imetangaza kupiga marufuku kwa muda mazishi ya serikali huku kukiwa na ukosoaji juu ya kupanda kwa gharama za maziko hayo.

Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah pekee ndiye aliye na uwezo wa kusema maziko yafanyike, serikali imesema.

Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Emma Theofelus alitoa tangazo hilo kufuatia kikao cha Baraza la Mawaziri mapema wiki hii.

Alisema kusitishwa kutaendelea hadi Aprili 2026, wakati kamati ya ukaguzi inaangalia “vigezo na michakato inayohusiana kufanyika kwa mazishi hayo.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *