Msomera wapewa elimu ya kuipa thamani mifugo

Msomera wapewa elimu ya kuipa thamani mifugo

Wafugaji katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga wamepewa elimu ya kunenepesha mifugo ili kupata mazao bora ya nyama.

Akitoa elimu afisa Mifugo Festo Nzalallila amewaomba wafugaji kufuata taratibu za ufugaji na malisho sahihi ya mifugo yao ili kupata mazao mazuri ya nyama ambapo amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo kutaongeza soko la biashara hiyo ya mazao ya nyama ndani na nje ya nchi.

Aidha afisa huyo wa mifugo amewambia wananchi wa Msomera kuwa eneo hilo kwa ufugaji na malisho ni zuri hivyo anaimani mazao ya nyama yatakuwa bora na kuwafikia walaji wa nyama kutoka Msomera.

Vilevile amewasisitiza wafugaji hao kuwa ni vyema wakafanya ufugaji wa kisasa ambao matokeo yake ni mazuri kibiashara huku akigusia suala la unenepeshaji wa mifugo ili kupata mazao bora ya nyama.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *