Mkutano wa Rais wa Marekani Donald Trump na mgeni wake Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine umeishia katika mzozo wa maneno kati ya Marais hao katika Ikulu ya Marekani na kuvunjika bila suluhu kuhusu kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine.
Katika mazungumzo hayo, Trump amemwambia Zelensky kuwa asiwe mbishi katika kufikia makubaliano ya kusitisha vita hiyo iliyodumu kwa miaka mitatu na badala yake aishukuru Marekani.
” Haushindi vita hii,”
” Isingekuwa msaada wa kijeshi wa Marekani tuliokupa, vita hii ingekuwa imeisha ndani ya wiki tatu,” Trump alimwambia Zelensky huku wakibishana.
” Akijibu kwa hasira, Rais Zelensky alisema;
“Sio wiki tatu, Rais wa Urusi ( Putin) yeye alisema vita hii ingeisha ndani ya siku tatu,”
” Toka vita imeanza, tumekuwa tukipambana wenyewe kuilinda nchi yetu,” alisema Zelensky, kauli ambayo haikumfurahisha Trump na kumwambia kuwa hana shukran kwa msaada aliopewa.
Mazungumzo yao yaliishia njiani na Trump kumtaka Zelensky aondoke na arudi tena kama ana nia ya kumaliza vita hiyo.
Trump alimwambia Zelensky kuwa anacheza na maisha ya watu na angeweza kusababisha vita ya tatu ya Dunia.
Hata hivyo, Rais Zelenskyy alimshukuru Rais wa Marekani Donald Trump, kufuatia majibizano makali katika Ofisi ya Oval, Februari 28, 2025.
Mkutano wa Ikulu ya White House kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy uliolenga kupata makubaliano ambayo yangeruhusu Marekani kupata haki adimu za madini ya Ukraine uligeuka kuwa mechi ya kelele kati ya viongozi hao wawili huku Trump akimtishia Zelensky “Utafanya makubaliano au tunatoka.” Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii kufuatia mkutano huo, Trump alionyesha kuwa makubaliano hayo yamezimwa.
“Nimeamua kuwa Rais Zelenskyy hayuko tayari kwa Amani ikiwa Amerika itahusika, kwa sababu anahisi kuhusika kwetu kunampa faida kubwa Urusi,” alisema.

