Msaidizi wa Vladimir Putin amepuuza madai ya usitishaji vita wa muda mfupi na Kyiv, akisema “si chochote ila ni mpango wa muda” kwa Ukraine.
Haya yanajiri wakati mjumbe wa Donald Trump Steve Witkoff akiwa mjini Moscow kabla ya mazungumzo ya Marekani na Urusi kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano kwa siku 30.
Wakati huo huo, jeshi la Urusi limesema kuwa limeuteka tena Sudzha, mji muhimu katika eneo la Kursk ambao hapo awali ulichukuliwa na vikosi vya Ukraine.
Hapo awali Ikulu ya Kremlin ilisema ilikuwa hatua ya mwisho ya operesheni ya kuiondoa Ukraine kutoka eneo ililoliteka kuvuka mpaka.
Putin alifanya ziara ya kushtukiza huko Kursk Jumatano. Mkuu wa jeshi la Ukraine, Oleksandr Syrsky, pia alisema kuwa baadhi ya wanajeshi wake walikuwa wakiondoka Kursk.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema nchi hiyo “imedhamiria” kufanya kazi “haraka iwezekanavyo” na washirika wake kuelekea amani.
