Malkia wa urembo Chidimma Adetshina, ambaye amekuwa katika utata wa utaifa wake, atanyang’anywa utambulisho wake wa Afrika Kusini na hati za kusafiria.
Idara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilianza kuchunguza kesi yake baada ya kuwa mshiriki wa fainali katika shindano la Miss Afrika Kusini, lakini alikosolewa huku watu wakihoji kuwa hakustahili kushiriki kwa sababu mama yake ana asili ya Msumbiji na baba yake ni Mnigeria.
Alijiondoa kwenye shindano hilo mwezi Agosti baada ya idara hiyo kutangaza kwamba mamake huenda alifanya udanganyifu kuwa alikuwa wa raia wa Afrika Kusini.
Bi Adetshina, mwanafunzi wa sheria, alishinda Miss Universe Nigeria baada ya kualikwa kushiriki na waandaaji.

