Lionel Messi ameaga rasmi timu ya taifa ya Argentina baada ya kuisaidia kuifunga Benin mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Monumental nchini Argentina.
Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa Messi kuichezea Argentina. Alitoa pasi mbili zilizozaa mabao kabla ya kufunga bao la tatu.
Katika miaka 21 akiwa na timu ya taifa, Messi amecheza mechi 208, akifunga mabao 126 na kutoa pasi 70 za mabao.
Messi alianza kuichezea Argentina mwaka 2005. Akiwa na timu hiyo, alishinda kombe la Dunia la U-20 mwaka 2005, medali ya dhahabu ya Olimpiki mwaka 2008, Copa América mara mbili mwaka 2021 na 2024, Kombe la Dunia mwaka 2022 na Finalissima mwaka huo huo.
Katika ngazi ya klabu, Messi amewahi kucheza FC Barcelona, Paris Saint-Germain na Inter Miami ya Marekani. Mafanikio yake katika soka yamemsaidia kushinda tuzo ya Ballon d’Or mara nane.

