Mchengerwa atengua kauli ya Chalamila kuhusu mwendokasi

Mchengerwa atengua kauli ya Chalamila kuhusu mwendokasi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Mohamed Mchengerwa, ametengua kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Albert Chalamila iliyokuwa inaruhusu vyombo vya usafiri kutumia barabara za mabasi yaendayo haraka maarufu mwendokasi.

Amesema barabara hizo zinaharibika kwa matumizi yasiyo sahihi ikiwemo kutumiwa na malori yenye uzito.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya DMDP awamu ya Pili ya ujenzi wa barabara katika Halmashauri tano za Dar es Salaam na kubainisha kuwa barabara ya mwendokasi ya Mbagala imeanza kuharibika kutokana kutumiwa na magari yenye uzito mkubwa.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *