Mbabe Foreman afariki dunia

Mbabe Foreman afariki dunia

Bingwa wa zamani wa uzani wa juu George Foreman, ambaye alishindwa na Muhammad Ali katika mchezo wa ndondi maarufu wa 1974 “Rumble in the Jungle” kabla ya kutwaa tena taji hilo miongo miwili baadaye, amefariki Ijumaa akiwa na umri wa miaka 76, familia yake ilisema.

Foreman anayejulikana sana kama Big George, aliacha shule akiwa kijana na kuwa bingwa wa Olimpiki na baadaye gwiji wa ndondi.

Alipigana mara 81, akishinda 76, 68 kati ya hizo kwa mtoano ( knock-out).

Mbali na ndondi, Foreman alionekana katika matangazo ya TV na kuwa mtu mashuhuri nje ya mchezo huo.

“Kwa huzuni kubwa tunatangaza kufariki kwa mpendwa wetu George Edward Foreman Sr, ambaye alifariki kwa amani Machi 21, 2025, akiwa amezungukwa na wapendwa,” familia ya Foreman ilisema katika taarifa kwenye Instagram.

“Tunashukuru kwa kumiminiwa upendo na maombi,”

” Tunaomba faragha tunapoheshimu maisha ya mtu ambaye tulibarikiwa kuwa naye .”, iliongeza familia yake.

Promota mashuhuri wa ndondi Bob Arum alimpigia saluti Foreman kama “mmoja wa wapiga ngumi na watu mashuhuri ambao mchezo wa ngumi unajivunia”

Akiwa mzaliwa wa Texas mnamo Januari 10, 1949, Foreman alikulia huko Houston.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *