Manchester United tayari wamefanya mazungumzo na wagombea kadhaa wa umeneja huku shinikizo zaidi likizidi kupanda kwa Mholanzi Erik ten Hag, huku Xavi Hernandez na Ruben Amorim wa Sporting Lisbon wakiwa miongoni mwa wanaotajwa kurithi kiti hicho.
Ten Hag amekuwa na wakati mgumu United baada ya mwenendo usioridhisha.
Kwa mujibu wa tetesi kutoka gazeti la Daily Mail, makocha kadhaa tayari wanafikiriwa kuchukua nafasi yake.

