Manchester United wamechezea kichapo cha 2-1 kutoka West Ham United katika Ligi ya Uingereza.
Jarrod Bowen alifunga penalti ya dakika za mwisho iliyozua utata na kuinua West Ham United katika ushindi huo.
Crysencio Summerville alifunga bao lake la kwanza akiwa na jezi ya West Ham waliopanda hadi nafasi ya 13 kwenye jedwali wakiwa na pointi 11 baada ya michezo tisa, sawa na Manchester United walio nafasi ya 14.
Ingawa kupoteza kwa Man United ni mara ya pili katika mechi 10 za michuano yote, matokeo haya bado yanampa presha meneja Erik ten Hag kwa mara nyingine tena.
“Mara tatu katika msimu tunahisi kuonewa” Ten Hag aliiambia BBC.
“Ilikuwa lazima tufunge, tumetengeneza nafasi nyingi sana lakini hatukupata matokeo,” amesema.

