Magwiji Eto’o, Adebayor waibukia Somalia

Magwiji Eto’o, Adebayor waibukia Somalia

Magwiji watatu wa kandanda barani Afrika – Samuel Eto’o, Emmanuel Adebayor na Jay-Jay Okocha – wameshuka uwanjani nchini Somalia Jumanne kwa ajili ya mechi ya maonyesho inayolenga kurejesha furaha nchini humo.

Mastaa hao watatu walikuwa sehemu ya “ziara ya amani” inayoungwa mkono na Fifa ambayo Somalia inatumai itaisaidia kwa mara nyingine kuandaa mechi za kimataifa.

Somalia imekuwa katika hali ya migogoro ya mara kwa mara ya ndani tangu 1991 na timu yake ya taifa imelazimika kucheza mechi nyingi katika nchi jirani ya Djibouti.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *