Maelfu ya wakimbizi wanakabiliwa na njaa Kenya

Maelfu ya wakimbizi wanakabiliwa na njaa Kenya

Mamia ya maelfu ya watu “wanakabiliwa na baa la njaa katika kambi za wakimbizi za Kenya baada ya kupunguzwa kwa ufadhili wa Marekani kupunguza mgao wa chakula hadi viwango vyao vya chini kuwahi kutokea, afisa wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC.

Athari hiyo inaonekana wazi katika hospitali katika kambi ya Kakuma kaskazini-magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kenya kumekuwa ni nyumbani kwa takriban wakimbizi 300,000 ambao wamekimbia mapigano katika nchi barani Afrika na Mashariki ya Kati.

Watoto waliodhoofika wanajaza wodi ya vitanda 30 katika Hospitali ya Amusait ya Kakuma, wakiwatazama wageni bila kuongea huku wakipokea matibabu ya utapiamlo mbaya sana.

Mtoto mmoja, Hellen, anaonekana kudhoofika .

Sehemu za ngozi yake zimekunjamana na kuchubuka, na kuacha mabaka mekundu – yakiwa ni matokeo ya utapiamlo, daktari aliiambia BBC.

Katika orodha hiyo, kuna mtoto mchanga wa miezi tisa, James, mtoto wa nane wa Agnes Awila, mkimbizi kutoka kaskazini mwa Uganda.

“Chakula hakitoshi, watoto wangu wanakula mara moja tu kwa siku. Kama hakuna chakula unawalisha nini?” anauliza.

James, Hellen na maelfu ya wakimbizi wengine huko Kakuma wanategemea Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa msaada wa chakula.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *