MAAJABU YA LISBON: Sporting CP Yapindua Meza, Yaibamiza Bodo/Glimt 5-0 na Kutinga Robo Fainali

MAAJABU YA LISBON: Sporting CP Yapindua Meza, Yaibamiza Bodo/Glimt 5-0 na Kutinga Robo Fainali

Mabingwa wa Ureno, Sporting CP, wameandika historia ya aina yake baada ya kufanya mapinduzi makubwa (comeback) na kuiondosha Bodo/Glimt ya Norway kwa ushindi wa kishindo wa 5-0 (Jumla ya mabao 5-3) baada ya dakika 120 za mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mchezo Ulivyokuwa: Kutoka 3-0 hadi 5-3 Sporting waliingia uwanjani wakiwa na deni la mabao 3-0 kutoka mchezo wa kwanza, lakini wakiongozwa na mashabiki wao, walionyesha ari ya hali ya juu:

  • Dakika ya 34: Goncalo Inacio alifungua karamu ya mabao kwa kichwa safi akimalizia kona ya Francisco Trincao.
  • Dakika ya 61: Pedro Goncalves alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi ya Luis Suarez, na kuifanya Sporting kuhitaji bao moja tu kusawazisha jumla ya mabao.
  • Dakika ya 78: Baada ya ukaguzi wa VAR, Sporting walipata penalti iliyofungwa kiufundi na Luis Suarez, na kufanya matokeo kuwa 3-3 kwa jumla na kupeleka mchezo kwenye muda wa ziada (extra time).

Muda wa Ziada na Kipigo cha Mbwa Mwizi Sporting walihitaji dakika mbili tu za muda wa ziada kumaliza kazi:

  • Maxi Araujo alifunga bao la nne lililowapa uongozi wa jumla kwa mara ya kwanza.
  • Kijana mdogo aliyengia akitokea benchi, Rafael Nel, alipigilia msumari wa mwisho dakika za mwisho na kuhitimisha ushindi wa 5-0 (5-3 Aggregate).

Bodo/Glimt, ambao walishangaza ulimwengu kwa kuzifunga timu kama Manchester City na Atletico Madrid katika safari yao, wameishia hatua ya 16 bora huku Sporting wakisonga mbele kwa mara ya kwanza katika hatua ya robo fainali baada ya miaka mingi.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *