Kikwete ashiriki kutoa mafunzo kwa Mawaziri Marekani

Kikwete ashiriki kutoa mafunzo kwa Mawaziri Marekani

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho yupo Boston, Marekani ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wakiwemo wa Fedha na wa Mipango kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Ngazi ya Mawaziri wa Harvard “Harvard Ministerial Leadership.

Program hiyo inaendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard.

Mheshimiwa Rais Mstaafu ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu wanaoshiriki kutoa mafunzo hayo.

Pamoja na Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu, wengine wanaoshiriki kutoa mafunzo hayo ni pamoja na Wakuu wa Taasisi za Kimataifa, Mashirika Binafsi na Wabobezi katika masuala ya sera, uchumi na maendeleo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *