Waziri wa ulinzi wa Israel amesema kuwa kiongozi mkuu wa Iran anapaswa kulaumiwa baada ya shambulio la kombora la Iran kwenye hospitali.
Hata hivyo, vyombo vya habari vya serikali ya Irani vimeripoti kwamba shambulio la kombora lililenga eneo la kijeshi karibu na hospitali kusini mwa Israeli, na sio kituo chenyewe.
Makumi ya watu wameripotiwa kujeruhiwa baada ya Iran kurusha safu ya makombora usiku kucha.
Mashambulizi hayo asubuhi ya leo yanakuja katika wakati mgumu, huku Donald Trump akizingatia uwezekano wa Marekani kuhusika moja kwa moja katika kuisadia Israel.
Trump ameripotiwa kuidhinisha mipango ya kushambulia Iran, lakini hajafanya uamuzi wa mwisho.

