Israel kuendelea kuikalia Gaza hata vita vikiisha

Israel kuendelea kuikalia Gaza hata vita vikiisha

Waziri wa ulinzi wa Israel amesema wanajeshi watasalia katika ukanda wa Gaza katika kile kinachoitwa kulinda usalama kwa kuyateka maeneo makubwa ya Gaza hata baada ya kumalizika kwa vita.

Israel Katz alisema maeneo hayo yatatoa “kinga” kulinda jamii za Israel “katika hali yoyote iwe kwa muda mfupi au muda mrefu .

Israel itaendelea na mzingiro wake wa wiki sita wa misaada ya kibinadamu ili kuishinikiza Hamas kuwaachilia mateka, alisema, licha ya onyo la Umoja wa Mataifa .
Siku ya Jumatano Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) lilipaza sauti kutokana na athari za kampeni ya Israel, likisema kwamba Gaza “imegeuzwa kuwa kaburi la umati wa Wapalestina na wale wanaokuja kuwasaidia.

“Tunashuhudia kwa wakati halisi uharibifu na mauaji kwa wakazi huko Gaza,” Amande Bazerolle, mratibu wa dharura wa shirika la misaada huko Gaza, alisema.

Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema zaidi ya watu 1,650 wameuawa tangu vita kuanza tena tarehe 18 Machi.

Maafisa wa hospitali walisema takriban Wapalestina 24 waliuawa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza siku ya Jumatano.

Wengi wa walioripotiwa kuuawa walikuwa katika mji wa Gaza, kaskazini mwa nchi hiyo.

Walijumuisha watu 10 wa familia ya Hassouna, wengi wao wakiwa watoto na wanawake. Mmoja wao alikuwa Fatema Hassouna – mwandishi mchanga na mpiga picha anayechipukia.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *