Iran yahofiwa kuendelea kuwa tishio

Iran yahofiwa kuendelea kuwa tishio

Iran ina uwezo wa kuanza kurutubisha madini ya uranium tena – kwa uwezekano wa kutengeneza bomu – katika “muda wa miezi kadhaa”, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya nyuklia amesema.

Rafael Grossi, mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ( pichani) alisema mashambulizi ya Marekani katika maeneo matatu ya Iran mwishoni mwa juma lililopita yamesababisha uharibifu mkubwa lakini sio kwa kiasi kikubwa, kinyume na madai ya Donald Trump kwamba vifaa vya nyuklia vya Iran “vimeangamizwa kabisa”.

“Kusema ukweli, mtu hawezi kudai kwamba ameharibu miundombinu ya nyuklia ya Iran,” Grossi alisema Jumamosi.

Israel ilishambulia maeneo ya nyuklia na kijeshi nchini Iran tarehe 13 Juni, ikidai kuwa Iran ilikuwa karibu kutengeneza silaha za nyuklia.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *