Waziri wa Maji na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Pangani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Juma Aweso amesema Serikali ina mpango wa kutumia mfumo mpya wa malipo ya huduma ya maji utakaofahamika kama “LUKU ya Maji” ili kumfanya mwananchi alipie kadri anavyotumia kama ilivyo katika mfumo wa kununua umeme.
Aweso ameutaja mpango huo mbele ya Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Kinyerezi, Ilala – Dar es Salaam.
Aweso aliongeza kuwa ujio wa mfumo huo ni matokeo ya maono na uongozi thabiti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuboresha sekta ya maji ili kuondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa Watanzania.
Mpango huu amesema utatekelezwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

