Harris: Sikumshawishi Biden kutogombea Urais

Harris: Sikumshawishi Biden kutogombea Urais

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ( kulia pichani) amefichua siri kuwa hakuwahi kumuomba aliyekuwa Rais wa wakati huo Joe Biden ( kushoto pichani) kujiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwania Ikulu ya Marekani kwa sababu ya uzee.

Katika mahojiano na BBC Jumapili na Laura Kuenssberg, alisema: “Najiuliza kama nilipaswa kuwa na mazungumzo naye na kumtaka asigombee tena uchaguzi,” amesema.

“Ninatafakari kama nilipaswa kuwa na mazungumzo naye kuhusu hilo na kumtaka asigombee tena uchaguzi ule kwa sababu ya umri wake”ameongeza.

Hata hivyo, baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu afya yake na akili yake kudaiwa kupoteza kumbukumbu , Rais Biden alishindwa kuwashawishi Wamarekani kumchagua tena Julai 2024 baada ya kushindwa katika mjadala dhidi ya Donald Trump.

Harris aliingia kama mgombe wa chama cha Democratic akichukua nafasi ya Biden, lakini akashindwa na Trump.

Harris ameyasema hayo katika kitabu chake kuhusu kampeni yake ya miezi mitatu kwamba hakujadiliana na Rais Biden kuwa alikuwa na wasiwasi juu ya uwezo wake.

” Kama ningefanya hivyo, basi ingeonekana mimi nautaka Urais,”

” Jambo hilo lilikuwa ni jambo binafsi,” amesema.

Hata hivyo, Biden aliyekuwa na miaka 80 wakati huo na kukumbwa na uvumi kuhusu afya yake ya akili baada ya kudaiwa kupoteza kumbukumbu, alipoteza matumaini ya kuchaguliwa tena baada ya kushindwa vibaya katika mjadala na Rais wa sasa Donald Trump.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *