Gamondi sasa aipigia hesabu JKT Tanzania

Gamondi sasa aipigia hesabu JKT Tanzania

Baada ya kuwafunga watani wao wa jadi Simba 1-0 katika dabi, kocha wa Yanga Miguel Gamondi sasa anaelekeza nguvu katika mechi yao nyingine ya Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania.

Mechi hiyo itachezwa kesho jioni katika uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Akiongea kuelekea mechi hiyo, Gamondi amesema;

“Tupo tayari tena kujianda na mchezo mwingine,”

“Tunakwenda kucheza na timu ambayo imepoteza mchezo mmoja na kutoka sare michezo minne, kimsingi wanaonekana ni wagumu lakini tunajua nini chakufanya,”

“Nafahamu msimu uliopita tulishinda magoli matano, walikuwa na timu tofauti na mwalimu tofauti,”

” Kwangu mimi sitazami yaliyopita. Yaliyopita yamepita natazama yajayo, nimewaona wanavyocheza msimu huu wapo vizuri hivyo nakwenda kucheza nao kwa namna wanavyocheza na sio kutazama awali walikuwaje”, amesema.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *