Galatasaray imetwaa taji la 25 la Uturuki huku ikiwa imesalia na michezo miwili mkononi kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Kayserispor siku ya Jumapili.
Ushindi huo uliifanya Galatasaray kuongoza kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya wapinzani wao wakuu wa Istanbul Fenerbahce, ambao hawajashinda ligi kwa zaidi ya muongo mmoja.
Galatasaray wapo kileleni wakiwa na pointi 89 na Fenerbahce, ambao waliilaza Eyupspor 2-0 Jumapili wakifuatia wakiwa na pointi 81.
Samsunspor wanashika nafasi ya tatu kwa pointi 60.
Mshambulizi wa Nigeria, Victor Osimhen alifunga bao la kwanza dakika ya 26 akifuatiwa na winga wa Uturuki Baris Alper Yilmaz dakika tatu baadaye kipindi cha kwanza.

