Fernandes aongeza mkataba Man Utd hadi Juni 2027

Fernandes aongeza mkataba Man Utd hadi Juni 2027

Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes ametia saini kandarasi mpya itakayomweka katika klabu hiyo hadi Juni 2027, kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine, klabu hiyo ya Ligi ya Premia imesema.

Kiungo huyo wa kati wa Ureno ambaye alijiunga na United mwaka 2020, amefunga mabao 79 na kutoa asisti 67 katika mechi 234 alizoichezea klabu hiyo.

Mchezaji huyo alikuwa amesaini mkataba wa awali mwaka 2022 uliodumu hadi 2026.

“Kila mtu anajua mapenzi niliyo nayo kwa Manchester United,” mchezaji huyo wa miaka 29 alisema katika taarifa yake.

“Ninaelewa jukumu na umuhimu wa kuvaa shati hii, nahitaji kujitolea katika kuichezea klabu hii,” amesema.

Mabingwa hao wa Kombe la FA United wanaanza kampeni zao za Ligi Kuu ya Uingereza wakiwa nyumbani Ijumaa dhidi ya Fulham.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *