ETHIOPIA YAPOKEA NDEGE 12 ZA KIVITA KUTOKA URUSI KATIKATI YA MAPIGANO TIGRAY

ETHIOPIA YAPOKEA NDEGE 12 ZA KIVITA KUTOKA URUSI KATIKATI YA MAPIGANO TIGRAY

Ethiopia imepokea shehena ya ndege 12 za kivita za kisasa aina ya Su-35 kutoka nchini Urusi, hatua inayokuja wakati mapigano yakizidi kupamba moto katika eneo la Tigray, kaskazini mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Eritrea.

Akizungumza akiwa nchini Urusi kwenye Mkutano wa Kilele wa Urusi na Afrika jijini Moscow, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, alieleza kuwa kuwasili kwa ndege hizo mapema kuliko ilivyotarajiwa ni hatua kubwa katika kuimarisha uwezo wa ulinzi wa taifa lake. Alibainisha kuwa hatua hii ni matokeo ya mkataba wa ushirikiano wa kisheria na wa kijeshi uliotiwa saini kati ya mataifa hayo miaka kadhaa iliyopita.

Mbali na ndege hizo, Abiy alifichua mipango ya Ethiopia kununua mifumo minne ya ulinzi wa anga aina ya S-400 kutoka Moscow ili kujilinda dhidi ya chokochoko na vitisho kutoka nje.

Akimsifu Rais Vladimir Putin kama “rafiki wa dhati wa Ethiopia,” Waziri Mkuu huyo alisisitiza kuwa ununuzi huu unaifanya Ethiopia kuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara kumiliki zana hizo zenye teknolojia ya hali ya juu. Ushirikiano huu unazidi kuimarika kufuatia mikataba mbalimbali ya kijeshi waliyowekeana hivi karibuni, ikiwemo ule wa mwaka 2021 unaohusu mafunzo ya wanajeshi na uboreshaji wa zana za kivita.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *