Email ya maoni Rais kuongezewa muda Kenya yazidiwa

Email ya maoni Rais kuongezewa muda Kenya yazidiwa

Anwani ya barua pepe iliyotolewa kwa umma kutoa maoni yao kuhusu sheria zilizopendekezwa katika Seneti ya Kenya imekwama baada ya kuzidiwa na majibu mengi.

Mswada huo unalenga kuongeza muda wa kukaa ofisini kwa rais, magavana wa kaunti na wabunge kutoka miaka mitano hadi saba, miongoni mwa marekebisho mengine ya katiba.

Mpango huo ulikabiliwa na hasira ya umma na Wakenya wamekuwa wakihamasishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Baraza la juu la bunge la nchi hiyo lilipokea zaidi ya “mawasilisho 200,000, yaliyofikia kiwango cha juu”, ilisema chapisho kwenye akaunti ya X ya Seneti.”

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *